Breaking News

Tuesday, July 19, 2016

Video: Makomando – Wanachezaje


8d831c0d-911d-4065-bf0d-4c6b4012ab90
Video mpya kutoka kwa kundi la Makomando, wimbo unaitwa “Wanachezaje”, video imeongozwa na Joowzey & Shevi Issa.

Read more ...

Jokate ameamua kusifia kitu hiki kutoka kwa Diamond..

jokateee
Diamond Platnumz anazidi kuwa karibu tena na maex wake. Jacqueline Wolper, Wema Sepetu hawana noma naye tena – na sasa Jokate Mwegelo!
Ya Jokate ina nguvu zaidi kwakuwa kwa sasa ana uhusiano na hasimu wake kiburudani, Alikiba na hiyo ni ishara kuwa uadui kati ya Diamond na Kiba umebaki kwa mashabiki tu.
Mrembo huyo amempongeza Diamond kwa uwezo wake mkubwa wa uchezaji wa style mpya kwenye hit single yake, Kidogo.
Jokate
Akipost kipande cha video Instagram kikimuonesha Diamond na dancers wake wakifanya mazoezi kwa wimbo huo, Jokate ameandika: You just took choreography ya East African tracks to another sphere, inspirational is an understatement. Moves za kwenye huu wimbo. I can’t even hata.”
Jojo pia anatamani amuone Chibu na Kiba kwenye ngoma moja.
“Naendelea kusubiri siku utakayo fanya kazi na team kiba tho- kiroho safi 😊. Hongera kwa kazi nzuri dogo @diamondplatnumz.”
Mapokezi ya post hiyo yana mchanganyiko wa hisia. Ila wengi wamempongeza.
Mara ya mwisho Jokate anamuongelea Diamond ilikuwa ni malalamiko aliyommwagia kwa kumuita mswahili na mdhalilishaji wa wanawake.
Chanzo: Bongo5
Read more ...

Audio: Chid Benz na Rayvany wametuletea huu mdundo ‘Chuma’

Chid & RaymondBaada ya kimya kirefu mkali wa midundo ya Hiphop nchini Chid Benz, anatualika kwenye ngoma yake mpya ya ‘Chuma’ aliyomshirikisha Rayvany kutokaWCB, ngoma iliyotayarishwa na proudcer Laizer pamoja na Mr T Touch

Read more ...

Ndugu wa mtanzania aliyewekwa rehani kwa unga Pakistan wazungumza


IMG_20160719_112117
Baada ya wiki hii katika mitandao ya kijamii kusambaa video inayomuonyesha kijana mtanzania anayedaiwa kuwekwa rehani nchini Pakistan kutokana biashara ya unga, ndugu wa kijana huyo anayetambulika kwa jina la ‘Adamu Akida’ wamezungumza.
Akiongea na gazeti la Mtanzania kaka wa Adamu aliyejitambulisha kwa jina la Hemed Abdallah (si jina lake halisi) alisema miezi minane iliyopita, Adamu alikwenda kwa kaka yake ambaye ni mtoto wa mama yake mdogo aliyetambulika kwa jina la Juma, na kuomba msaada wa mtaji kwani kazi yake ya kinyozi haikuwa ikilipa na hali ya maisha ilikuwa ngumu.
Alisema baada ya kueleza shida yake hiyo, kaka yake huyo (Juma) alimuhoji kama yupo tayari kwa ajili ya kutafuta maisha nje ya nchi, na Adamu alikubali kufanya kazi ya aina yoyote ili mradi aweze kupata pesa.
“Adamu kwa sasa ameshikiliwa kwa muda wa miezi minane, hatujui kama alikuwa ameingia katika janga hili hadi pale tulipoona video zake katika mitandao ya kijamii. Hapa aliyepo ni baba yake mdogo, Kessy Baharia na baba yake mzazi yupo Bagamoyo Mlingotini, ndiko anakoendelea na maisha yake.
“Awali alikwenda kwa kaka yake mtoto wa mama yake mdogo anaitwa Juma na kuomba asaidiwe mtaji kwani amekuwa na maisha magumu sana. Baada ya hali hiyo aliambiwa kuna safari ya kwenda Pakistan ambayo waliondoka wakiwa wameambatana watu watatu pamoja na Juma na kijana mwengine ambaye jina lake limenitoka, ila anaishi Kinondoni.
“Walipofika kule, Juma akachukua mzigo akiwa na yule kijana wa Kinondoni, huku Adamu akiachwa Pakistan kwa maelezo kuwa baada ya siku tano atakuja nchini na mzigo mwingine. Muda wote hata tukihoji alipo Adamu tunaambiwa yupo anaendelea na kazi huko aliko ana angerudi mwezi wa tisa nane.
“Sasa hii video ndiyo imetupa picha halisi ya Adamu, maskini sijui kama tutampata akiwa hai. Hata hivyo kwa kipindi cha hivi karibuni, tulikuwa tukishangazwa na mwenendo wa Juma kwani amekuwa na fedha nyingi sana hadi kufikia kuwajengea nyumba dada zake pamoja na kuwanunulia magari,” alisema Abdallah huku akibubujikwa na machozi.
Mke wake
Inaelezwa kuwa mke wa Adamu ambaye alikuwa akiishi Mtaa wa Sunna, Magomeni, alihamia Kijitonyama.
Kwamba alihamishwa na shemeji yake, Juma ambaye ndiye aliyempangia nyumba nyingine Kijitonyama.
“Katika suala hilo, tuna shaka kuwa hata mke wa Adamu anajua kinachoendelea, maana miezi mitatu iliyopita alihama Magomeni na kuhamia Kijitonyama, tena huku akisema mume wake karibu anarejea nchini.
“Lakini baada ya video kuanza kuonekana, sasa hata kupatikana hapatikani, na hatujui amehamia nyumba gani huko Kijitonyama,” alisema Abdallah.
Serikali ya Mtaa
Akizungumza na Mtanzania, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Idrissa, Issa Mpangile, alisema kuwa jana askari kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi walifika katika ofisi yake na kumtaka waongozane kwenda katika nyumba ya baba mdogo wa Adamu.
Alisema walipofika nyumbani kwa Kessy Baharia, ambaye ndiye baba mdogo wa Adamu, polisi walichukua maelezo yake na baadaye wakarudi katika ofisi ya Serikali ya Mtaa kuchukua maelezo ya mwenyekiti huyo.
Akizungumza kuhusu kijana huyo, Mpangile alisema kuwa ni mzaliwa wa mtaa huo, lakini baadaye alihamia Mtaa wa Suna ambao ni jirani na Mtaa wa Idrissa, Kata ya Magomeni.
Alisema wakati kijana huyo anahama mtaa huo, alikuwa bado ni kinyozi na hakuwa na rekodi ya kusafiri kwenda nje ya nchi.
“Wakati Adamu anahama Mtaa wa Idrissa, alikuwa bado ni kinyozi na hakuna rekodi kwamba alikuwa anasafiri nje ya nchi,” alisema Mpangile.
Alisema katika mazungumzo na Baharia, alimweleza kuwa amewasiliana na baba wa kijana huyo ambaye anaishi Bagamoyo mkoani Pwani.
Mpangile alisema kwa mujibu wa Baharia, baba wa kijana huyo anayejulikana kwa jina la Akida, amesikia habari za mtoto wake na kwamba atakwenda kuripoti kituo cha polisi.
Naye mama mdogo wa Adamu, aliyetambulika kwa jina la Khadija Katundu, alikiri maofisa wa polisi kumuhoji mume wake.
Alisema wameendelea kutoa ushirikiano kwa watu wanaofika nyumbani kuhoji kuhusu suala hilo, na kwamba wanaamini ufumbuzi utapatikana.
Serikali yahaha
Baada ya taarifa hizo kuripotiwa na gazeti hili jana, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Jeshi la Polisi wanafanya mawasiliano na Serikali ya Pakistan ili kuangalia namna ya kumwokoa Adamu katika mikono ya maharamia hao.
Akizungumza na MTANZANIA jana, Msemaji wa Polisi, Advera Bulimba, alisema tayari wamepata taarifa dhidi ya Mtanzania huyo.
“Kwa sasa tunafanya mawasiliano na wenzetu wa Pakistan tuone namna ya kumtoa kijana huyo katika mikono ya hao watekaji, na tukikamilisha hilo tutatoa taarifa rasmi juu ya jambo hili,” alisema Advera.
Wakati hayo yakiendelea, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, kupitia mmoja wa maofisa wa idara ya habari ambaye hakupenda kutajwa jina lake gazetini, alisema wamepata taarifa ya tukio hilo, na sasa wanafanya mawasiliano na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Source: Mtanzania
Read more ...

Monday, July 18, 2016

PICHA 22: List ya washindi wa tuzo 13 za Ligi Kuu Tanzania bara 2015/2016


Usiku wa July 17 2016 kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom ambayo ndio wadhamini wakuu wa Ligi Kuu soka Tanzania bara, walitangaza na kutoa tuzo 13 kwa wachezaji, refa na timu bora zilizofanya vizuri msimu wa 2015/2016,  Vodacom kwa kushirikiana na TFF wamefanikiwa kuchagua na kutoa zawadi kwa washindi wa tuzo hizo.
DSC_1657
Washindi wa tuzo Ligi Kuu katika picha ya pamoja na wageni waalikwa
List ya washindi wa tuzo na zawadi walizochukua
  • Mchezaji bora wa Ligi Kuu 2015/2016 ni Juma Abdul wa Yanga Tsh Milioni 9,228,820
  • Mchezaji bora wa kigeni ni Thabani Kamusoko wa Yanga Tsh Milioni 5,742,940
  • Mfungaji bora ni Amissi Tambwe wa Yanga Tsh Milioni 5,742,940
  • Mchezaji bora chipukizi ni Mohamed Hussein wa Simba Tsh Milioni 4.
  • Golikipa bora ni Aishi Manula wa Azam FC Tsh Milioni 5,742,940
  • Refa bora ni Ngole Mwangole Tsh Milioni 5,742,940
  • Kocha bora ni Hans van Pluijm wa Yanga Tsh Milioni 8.
  • Timu yenye nidhamu Mtibwa Sugar Tsh Milioni 17,228,820
  • Bingwa wa Ligi Kuu Yanga Tsh Milioni 81,345,723
  • Mshindi wa pili Azam FC Tsh Milioni 40,672,861
  • Mshindi wa tatu Simba Tsh Milioni 29,052,044
  • Mshindi wa nne Tanzania Prisons Tsh Milioni 23, 241,635
  • Mfungaji wa goli bora ni Ibrahim Ajib wa Simba Tsh Milioni 3
DSC_1532
Kocha wa Yanga Hans van Pluijm baada ya kutwaa tuzo ya kocha bora akisalimiana na waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba
DSC_1521
Kocha wa Yanga Hans van Pluijm akipokea tuzo ya kocha bora akiwa kaongozana na mkewe.
DSC_1536
Kocha wa Yanga Hans van Pluijm akisalimiana na Rais wa TFF Jamal Malinzi
DSC_1542
Mwameja akikabidhi tuzo ya golikipa bora kwa Aishi Manula wa Azam FC
DSC_1550 - Copy
Ibrahim Ajib akipokea mfano wa hundi ya Tsh Milioni 3 kama zawadi ya ufungaji goli bora.
DSC_1560
Thabani Kamusoko akiwa na mkewe na mtoto wake alipopokea mfano wa hundi ya Tsh Milioni 5 kama zawadi ya mchezaji bora wa kigeni.
DSC_1584
Kutoka kushoto ni Mohamed Hussein wa Simba ambaye ameshinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi.
DSC_1604
Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba akimkabidhi tuzo ya mchezaji bora wa Ligi Kuu Juma Abdul wa Yanga
DSC_1650
Kutoka kushoto ni mkuu wa masoko wa Yanga Omar, Juma Abdul na golikipa wa Yanga Deogratus Munish
DSC_1678
DSC_1690
DSC_1757
DSC_1386
DSC_1388
DSC_1395
DSC_1403
DSC_1417
DSC_1423
Kamusoko na familia yake
DSC_1430 - Copy
Chanzo: millardayo.com
Read more ...

Zeben aiongoza Azam FC katika mechi ya kwanza ikiichapa Ashanti

KOCHA Mkuu wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Zeben Hernandez, leo ameiongoza timu hiyo kwenye mchezo wa kwanza tokea akabidhiwe mikoba hiyo kwa kuichapa Ashanti United mabao 2-0.
Mchezo huo wa kirafiki wa kujiandaa na msimu ujao ulifanyika saa 3 asubuhi ndani ya dimba la Azam Complex, ambapo Zeben alipata fursa ya kukifanyia tathimini kikosi chake baada ya kuchezesha vikosi viwili tofauti kwenye kila kipindi cha mechi hiyo.
Ikiwa imefanya mazoezi kwa siku tisa chini ya makocha wapya kutoka Hispania, Azam FC inayodhaminiwa na Benki ya NMB ilijitahidi kumiliki mchezo huo, lakini ilishindwa kutumia nafasi takribani tano ilizotengeneza za kufunga mabao, ambapo ilishuhudiwa ikimaliza kipindi cha kwanza ikiwa imetoshana nguvu ya bila kufungana na wapinzani wake hao.
Mabadiliko ya kipindi cha pili aliyofanya Zeben ya kuingiza kikosi kingine, yazidi kuipa uhai zaidi Azam FC na hatimaye ikaweza kufunga mabao mawili mazuri ya kiufundi kupitia kwa viungo Mudathir Yahya na Abdallah Masoud ‘Cabaye’.
Mudathir ndiye aliyeanza kuziona nyavu za Ashanti United akifunga bao zuri dakika ya 69 kufuatia pasi safi ya Frank Domayo na kupiga shuti kali akiwa ndani ya eneo la 18 pembeni lililomshinda kipa Rajabu Hamisi.   
Cabaye alihitimisha ushindi huo kwa kufunga bao safi la pili akitumia vema pasi ya Ame Ally ‘Zungu’ dakika ya 81 na kupiga shuti kali akiwa umbali wa takribani mita 20 lililojaa wavuni na kuifanya Azam FC kuondoka na ushindi huo.
Katika mchezo huo benchi la ufundi la Azam FC lilipata fursa ya kuwajaribu wachezaji wawili waliokuwa majaribio, kipa Mhispania Juan Jesus Gonzalez aliyefuzu majaribio na mshambuliaji kutoka Ivory Coast, Ibrahima Fofana, ambao wote walicheza kipindi cha kwanza kabla ya timu nzima kubadilishwa kipindi cha pili.
Zeben aizungumzia mechi
Akizungumza na mtandao rasmi wa klabu www.azamfc.co.tz mara baada ya mchezo huo, Zeben ameeleza kufurahishwa kwa namna mchezo huo ulivyochezwa na viwango vya wachezaji wake, lakini hajafurahishwa na namna alivyowakosa baadhi ya nyota wake.
“Nimefurahishwa na viwango vya wachezaji wangu naamini itapelekea Azam FC kuwa na ubora mwakani, sijafurahishwa kuwakosa baadhi wachezaji wangu kama vile Shomari Kapombe (mgonjwa), Pascal Wawa (majeruhi) Kipre Tchetche na Farid Mussa anayeenda Hispania,” alisema.
Kocha huyo wa zamani wa Santa Ursula ya Hispania alisema kuwa amewaachia viongozi wa Azam FC kuhakikisha wanaziba mapengo hayo haraka iwezekanavyo, ambapo hivi sasa uongozi wa timu hiyo upo kwenye mchakato huo.
Mabao si ‘ishu’ hivi sasa   
Zeben alisema kwa sasa wanajaribu kuunda timu hiyo kwa kutatua matatizo yaliyopo kikosini, huku akidai kuwa katika mchezo wa leo walikuwa hawaangalii mabao bali eneo la ulinzi pekee na namna wachezaji wanavyocheza kwa nafasi.
“Tulikuwa tunaangalia eneo la ulinzi kwenye mchezo huu, tulikuwa hatuangalii sana mabao, mabao yalikuja kama kitu cha ziada tu, bado tupo kwenye kuunda timu na nasubiria uongozi ufanyie kazi mapengo hayo baada ya baadhi ya wachezaji kutokuwepo kikosini,” alisema.
Itamchukua mwaka wachezaji kuzoea mfumo
“Inaweza kuchukua mwaka mzima wachezaji kuuushika na kuuzoea mfumo wangu, kwa sasa tunaifanyia kazi Azam FC na wachezaji ni Azam FC, tunachofanya hivi sasa ni kupandikiza vitu vipya tulivyokuwa navyo kwa wachezaji taratibu kwa sababu wachezaji nao ni watu na huwezi kuwapa dozi kubwa.
“Itawachukua muda kidogo kuweza kuzoea falsafa yetu, kwani tupo kwenye kuivunja falsafa ya Uingereza waliyokuwa wanatumia msimu uliopita na kuingizia yetu ya Hispania, hivyo itachukua muda lakini ndicho tunachokifanyia kazi sasa hivi,” alisema.
Azungumzia majaribio ya Fofana, Gonzalez
Kocha huyo, 32, alisema kuwa Fofana si mchezaji mbaya kwa namna alivyomuaona kwenye mchezo wa leo huku akidai kuwa anahitaji kumwangalia zaidi katika muendelezo wa majaribio yake wiki ijayo inayoanza kesho Jumatatu.
“Kwanza ana heshima, anajifunza haraka anashirikiana vema na wenzake, lakini uamuzi zaidi wa majaribio yake utakuja wiki ijayo, lakini kwa sasa si mbaya,” alisema.
Zeben aliweka wazi kuhusiana na majaribio ya makipa Juan Jesus Gonzalez na Daniel Yeboah kutoka Ivory Coast, akidai kuwa Mhispania huyo amefuzu majaribio jana huku akimwelezea kuwa ni kipa mwenye kipaji kikubwa, ana mbinu kubwa na uwezo mkubwa wa kufikiri.
“Naamini ya kuwa kuwepo kwake kwa kushirikiana na makipa wengine, Azam FC itakuwa sehemu nzuri kwenye nafasi za juu na kudai kuwa makipa wote ni wazuri,” alisema.
Alisema kuwa ingekuwa ni uwezo wake angeweza kumchukua na kipa mwingine Yeboah aliyefeli majaribio, lakini kutokana na kuhitajika kwa nafasi moja ya kipa wa kigeni ameamua kumchagua Juan Jesus Gonzalez, huku akisisitiza kuwa makipa wote hao ni wazuri.
Baada ya mchezo huo wa kwanza wa kirafiki, Azam FC inatarajia kushuka tena dimbani Jumatano ijayo saa 3 asubuhi kuvaana na timu ya Halmashauri ya Kinondoni (KMC) kwenye mechi nyingine ya kujipima ubavu.
Kikosi cha Azam FC
Juan Jesus Gonzalez/Aishi Manula dk 46, Wazir Salum/Gadiel Michael dk 46, Erasto Nyoni/Abdallah Kheri dk 46, Aggrey Morris/Ismail Gambo dk 46, David Mwantika/Himid Mao dk 46, Michael Bolou/Frank Domayo dk 46, Jean Mugiraneza/Mudathir Yahya dk 46/Himid Mao dk 77, Salum Abubakar/ Abdallah Masoud ‘Cabaye’ dk 46, Ramadhan Singano/Khamis Mcha dk 46, Ibrahima Fofana/Kelvin Friday dk 46, Shaaban Idd/AmeAlly dk 46.
Read more ...

​Diamond asherehekea Kidogo kufikisha views milioni 1 ndani ya siku 4


Diamond Platnumz anasherehekea mafanikio ya video ya wimbo wake mpya, Kidogo.

Ndani ya siku nne, video ya wimbo huo aliowashirikisha P-Square imefikisha views zaidi ya milioni moja kwenye mtandao wa Youtube. Staa huyo hakusita kusherehekea hatua hiyo na mashabiki wake:
Video ya wimbo huo imetoka katika kipindi ambacho kundi la P-Square bado halina maelewano mazuri.i.
Chanzo: bongo5.com
Read more ...

Saturday, July 16, 2016

MSIKILIZE HAJI MANARA LIVE


Read more ...

YANGA WASAKA USHINDI WA KWANZA KOMBE LA SHIRIKISHO LEO

MABINGWA wa Tanzania Bara, Yanga SC leo watakuwa wanatafuta ushindi wa kwanza katika Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika, watakapomenyana na Medeama ya Ghana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Huo utakuwa mchezo wa mwisho wa mzunguko wa kwanza na wa tatu kwa washindi hao wa mataji yote Tanzania Bara, baada ya awali kufungwa mechi mbili, moja ugenini na moja nyumbani.
Yanga ilianza kwa kuchapwa 1-0 na Mouloudia Olympique Bejaia nchini Algeria kabla ya kufungwa 1-0 tena na TP Mazembe ya DRC mjini Dar es Salaam.
Na leo timu ya kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm inacheza mechi ya pili mfululizo nyumbani ikisaka ushindi wa kwanza, ili kurejesha matumaini ya kwenda Nusu Fainali.
Yanga SC watapigania ushindi wa kwanza Kombe la Shirikisho leo jioni

Kundi A

NaTimuPWDLGFGAGDPts
1TP Mazembe22004136
2Mouloudia Bejaia21101014
3Medeama201113-21
4Yanga SC200202-20

Kundi B

NaTimuPWDLGFGAGDPts
1Kawkab Marrakech22004226
2FUS Rabat21102114
3Etoile Sahel201123-11
4Al Ahly Tripoli200213-20

Katika mchezo wa leo, Yanga itawakosa wachezaji wake watatu tegemeo, beki wa kushoto Mwinyi Hajji Mngwali, viungo Deus Kaseke na Geoffrey Mwashiuya ambao wote ni majeruhi.
Aidha, Yanga itaendelea kumkosa beki wake mpya wa kulia, Hassan Kessy ambaye klabu yake ya zamani, Simba SC imegoma kumuidhinisha achezee klabu mpya.  
Mshambuliaji Mrundi, Amissi Tambwe alikuwa anasumbuliwa na Malaria kwa wiki yote hii, lakini tangu juzi amefanya mazoezi kikamilifu na wenzake, kuashiria kwamba anaweza kucheza leo.
Medeama iliyowasili Alhamisi Dar es Salaam nayo haijashinda mechi baada ya kufungwa ugenini na TP Mazembe 3-1 na kulazimishwa sare ya 0-0 nyumbani na MO Bejaia.
Bejaia wanatarajiwa kucheza kwa kushambulia leo, kwa sababu pamoja na kucheza ugenini lakini wanahitaji kushinda leo ili kufufua matumaini ya kwenda Nusu Fainali.
Kwa Yanga leo ni mtihani kweli kwa Pluijm aliyewahi kufundisha Medeama, kwani atahitaji kutafuta mabao na kujizuia kutoruhusu bao ili kukamilisha mpango wa kushinda mechi ya kwanza.
Mchezo mwingine wa kundi hilo utachezwa kesho, 
Mouloudia Bejaia wakiikaribisha TP Mazembe Uwanja wa Unite Maghrebine mjini Bejaia kuanzia Saa 3:45 usiku.
Mechi za Kundi B Kawkab Marrakech watakuwa wenyeji wa ndugu zao, FUS Rabat Uwanja wa Grand Marrakech, wakati Etoile Sahel wanaikaribisha Al Ahly Tripoli ya Libya leo Uwanja wa Olympique de Sousse, Tunisia.

Chanzo:http://www.binzubeiry.co.tz/
Read more ...
Designed By VungTauZ.Com