Breaking News

Saturday, June 29, 2013

MAANDALIZI YA HARUSI YA NATASHA, MONA AMFUNDA MAMA YAKE

Stori:Imelda Mtema
KAWAIDA mkubwa ndiyo humfunda mdogo lakini mambo yalikwenda kinyume kwa mwigizaji Yvonne-Cherry Ngatikwa ‘Monalisa’ ambaye alinaswa akimfunda mama yake mzazi, Suzan Lewis ‘Natasha’.
Tukio hilo lililopigwa chabo na paparazi wetu lilitokea hivi karibuni nyumbani kwa shosti wa Natasha aitwaye Nuru, Tandika Maghorofani, Dar wakati bi’mkubwa huyo alipokuwa akipewa somo (kufundwa) kabla ya kuitumikia ndoa inayotarajiwa kufungwa ‘soon’.
Wakati baadhi ya wafundaji tofauti wakiendelea kumfunda bi’mkubwa huyo mwenye umri wa miaka 46, ghafla Monalisa aliomba na yeye amfunde mama yake ambapo alianza kumshika mkono na kumpa ‘vipande’ vyake.
“Mh! Sasa jamani mama kufundwa na mwanaye wapi kwa wapi? Ninavyojua mimi mama ndiyo anaweza kumfunda mtoto sasa hii ya leo mpya,” alisikika msanii mkubwa aliyeomba hifadhi ya jina gazetini.
Shughuli hiyo iliyosheheni wageni waalikwa, ilitawaliwa na ngoma za asili kabla msafara kuelekea nyumbani kwa Natasha, Yombo jijini Dar.
CHANZO: GPL

No comments:

Designed By VungTauZ.Com