Breaking News

Tuesday, December 4, 2012

KOMBE LA UHAI KUANZA DESEMBA 7

Rais wa TFF, Leodegar Tenga

Na Prince Akbar
MICHUANO ya Kombe la Uhai inayoshirikisha timu za U20 za klabu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Desemba 7, mwaka huu kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Michuano hiyo, ambayo hudhaminiwa na Azam, watengenezaji na wasambazaji wa maji ya Uhai, inatarajiwa kufikia tamati Desemba 22 mwaka huu.
Ofrisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura Mgoyo ameiambia BIN ZUBEIRY mjini hapa kwamba, wachezaji watakaoshiriki michuano hiyo ni wale tu ambao usajili wao umefanyika TFF na kupatiwa leseni.
“Hakutakuwa na usajili mwingine wowote mbali na ule uliofanyika sambamba na wa Ligi Kuu. Taratibu zote za michuano hiyo zitafahamishwa kwa klabu husika ikiwemo ratiba ya michuano hiyo,”alisema ‘Big Bon’.

No comments:

Designed By VungTauZ.Com