KAMA
walivyo Wema Sepetu ‘Madam’ na Aunt Ezekiel kwa sasa ndivyo walivyokuwa
Wema na Kajala Masanja miezi kadhaa iliyopita.Wema na Kajala walikuwa
mashosti wa kufa mtu, walishibana na kupeana siri zao zote hususan zile
za ndani kabisa.
Kudhihirisha kwamba wameshibana, kuna wakati Wema aliamua kujitolea
Sh. Mil 13 kulipa faini ambayo ilimnusuru Kajala kuswekwa
gerezani.Baadaye walikuja kutofautiana, kila mtu akaishi kivyake.
Yakazungumzwa mengi kuhusu chanzo cha ugomvi wao lakini pointi ya msingi
ni kupishana kauli kibinadamu kama watu wengine wanavyoweza
kutofautiana na kupatana.
Kwa upande wao suala la kupatana limekuwa
zito, ugomvi wao haufiki tamati huku kila kukicha ni malumbano ambayo
yanawagawa mashabiki.
Tatizo kubwa linalochagiza ugomvi wao ni mitandao ya kijamii,
kumezuka makundi ambayo yamekuwa yakitumia utabiri wao wanaoufahamu
wenyewe kuzidi kuchochea ugomvi uliokuwepo kati ya mastaa hawa wawili na
wengine wakitumia matusi mpaka ya nguoni kutukana wa upande wa Wema na
Kajala.
Makundi hayo ndiyo yamekuwa chachu kubwa ya
bifu lao na kuzidisha mapambano kati ya mastaa hawa ambao naamini
wanapendana sana, sitaki kuamini kabisa kama Wema hampendi Kajala, na
sitaamini kama Kajala hampendi Wema.
Ndiyo maana siku ambayo walipatana na kuzungumza kwa muda nyumbani
kwa msanii Aunt Ezekiel, mastaa hao walipata fursa ya kukaa pamoja na
kuzungumza baada ya ugomvi wao kila mmoja alitoa chozi kuonyesha jinsi
gani kila mmoja anaumia anapokuwa mbali na mwenzake.
“Mimi nilikuwa napenda sana kukuangalia
wewe na siyo timu zinazotuzunguka zinazidi kututia chumvi tugombane,
nakupenda na ninajua ni rafiki mwema kwangu lakini unasikiliza sana
maneno ya watu,” ni maneno ya Kajala niliyosikia akimwambia Wema.
“Najua hivyo na wewe unafahamu nakupenda sana na ni rafiki ninayefurahi tukiwa pamoja nikiwa nawe siku zote,” alijibu Wema.
Maneno hayo waliyoambizana huku kila mmoja akitoa machozi,
yalisahaulika kwa siku tatu tu kwani viliibuka vitu ambavyo
havikujulikana vilipotokea na kuanzisha ugomvi mwingine mpya na
kuwafanya wawili hawa kuvurugana tena kwa kasi mpya na nguvu mpya.“Najua hivyo na wewe unafahamu nakupenda sana na ni rafiki ninayefurahi tukiwa pamoja nikiwa nawe siku zote,” alijibu Wema.
Nathubutu kusema kwamba ugomvi wa mastaa hawa mara nyingi unachagizwa na mitandao ya kijamii. Hizi zinazojiita Team Wema na Team Kajala ndiyo tatizo kubwa.Nasema ni tatizo kwa sababu hata ukiangalia kwa makini, kipindi cha nyuma mastaa hawa walipokuwa wanaanzisha urafiki wao, timu hizo hazikuwepo ndiyo maana waliweza kudumu.
Kwa nini wanakubali kutawaliwa na hizi Team? Kwa nini waruhusu maisha yao ya kila siku yaingiliwe uhuru wao wa kufanya mambo yao? Si sawa!
Mimi naamini kabisa kama mastaa hawa wangekuwa na ugomvi wao bila hizi Team kuingilia kati wangeweza kukaa pamoja na kumaliza tofauti zao mapema sana lakini tatizo kuna watu wa pembeni wenye kuzoa maneno huku na kupeleka kule.
Kwa jinsi ninavyoona mimi, hizi Team zikiendelea hivi na kwa mastaa wengine, ipo siku watasababisha hata mauaji kwa jambo ambalo halina kichwa wala miguu. Niwasihi Kajala na Wema wasijisahau kuwa wao ni biashara, mashabiki wengi wanapenda kuona kazi zao, wangeweka tofauti zao pembeni wafanye kazi na washirikiane hata kutengeneza filamu ya pamoja.
Naamini wakiweka pembeni hizi Team, wakaacha kusikiliza maneno ya kinafiki yanayoundwa na baadhi ya wasanii wasiopenda urafiki wao, basi wataishi vizuri na watafanya kazi zao pamoja!
Chanzo: GLP
No comments:
Post a Comment