Familia
kubwa inapokumbana na changamoto mbalimbali, baadhi ya wanafamilia
husambaratika na wengine huikabili kama sehemu ya mitihani ya maisha
iliyowapitia.
Mchanganyiko
mzuri wa wahusika wa Siri ya Mtungi, waliohusiana kwa damu au ndoa, au
kwa mapenzi tu, unaunda jamii inayohamasishwa na penzi, lililoletwa na
woga, ushirikina na usaliti, ikinyanyuliwa na ucheshi na furaha, na
kupewa nguvu ya mshikamano wa ndani wa familia na urafiki. Ni hadithi ya
mahusiano yaliyofaulu na yale yaliyopotea.
Ni hadithi ya mahusiano yaliyofaulu na yale yaliyopotea.
Kati
ya mitaa yenye harakati nyingi ya Dar es Salaam na ile iliyo kimya ya
Bagamoyo, tunapenya nyuma ya milango iliyofungwa mpaka kwenye maisha ya
Cheche na mkewe Cheusi, binti wa kiongozi maarufu mwenye wake wengi,
Mzee Kizito, pamoja na wahusika wengine kama Duma, mwana DJ; Lulu-
shangingi lililokubuhu; Farida- roho ya nyoka; Masharubu- mzee kikwekwe
na wengine wengi.
Cheche
anapozawadiwa studio ya biashara na marehemu Habibu, mpigapicha wa
Kiguru, anajikuta kuwa yeye si mpiga picha pekee bali ni kama alama au
kitovu cha kile watu wengine wanachokitaka kutoka katika maisha.
Mahusiano yake yakaanza kumletea matatizo.
Ndani
ya picha anazopiga watu mbalimbali, au familia na marafiki, Cheche
hukamata hisia mbalimbali za wanajamii zikionyesha matumaini, ndoto na
matatizo ya kibinafsi.
Usikose kuangalia tathmilia hii saa 3:30 usiku kila Jumapili kwenye ITV, na saa 3:30 usiku kila Jumatano kwenye EATV!





No comments:
Post a Comment