MABAO mawili yaliyofungwa na Jeremy Mathieu katika dakika ya 19 na
Luis Suarez dakika ya 56 yameipa ushindi timu ya Barcelona dhidi ya
mahasimu wao Real Madrid kwenye uwanja wao wa nyumbani Nou Camp usiku
huu.
Katika mtanange huo wa La Liga, Barcelona wametoka kifua mbele kwa mabao 2-1 dhidi ya Real Madrid.
Bao la Real Madrid limewekwa kimiani na Cristiano Ronaldo dakika ya 31 ya mchezo.
Kwa matokeo hayo, Barcelona wamefikisha pointi 68 mbele ya Real Madrid wenye pointi 64.


No comments:
Post a Comment