Wasichana
kutoka kata ya Ufukoni mkoani Mtwara wakisubiri kupatiwa elimu ya Afya
na uzazi na kugawiwa pedi kupitia mradi wa Hakuna Wasichoweza
unaoendeshwa na taasisi ya T-Marc chini ya ufadhili wa USAID na Vodacom
Foundation.Vodacom Foundation imeongeza $166,000 kwa ajili ya kuuongezea
nguvu mradi huo unaowalenga wasichana wanafunzi waliopo mashuleni na
wale wasio mashuleni na kwa kuanzia zoezi hili linafanyika katika mkoa
Mtwara.
Baadhi
ya wanafunzi wa shule ya msingi ya Mwenge iliyopo mkoani
Mtwara wakifurahi baada ya kugawiwa pedi za kujikinga wanapokuwa kwenye
hedhi.Mpango huo wa kuwagawia wasichana pedi na kuwapatia elimu ya Afya
na uzazi uko chini ya mradi wa Hakuna Wasichoweza unaoendeshwa na
taasisi ya T-Marc chini ya ufadhili wa USAID na Vodacom
Foundation.Vodacom Foundation imeongeza $166,000 kwa ajili ya kuuongezea
nguvu mradi huo unaowalenga wasichana wanafunzi waliopo mashuleni na
wale wasio mashuleni na kwa kuanzia zoezi hili linafanyika katika mkoa
Mtwara.Kutokana na mafanikio yaliyopatikana katika awamu ya kwanza ya mradi wa kuwawezesha wasichana wa Hakuna Wasichoweza, taasisi ya Vodacom Foundation imeongeza ufadhili wa Dola za Kimarekani 166,000 ili mradi uendelee na uweze kuwafikia wasichana 4,200 katika shule nyingine 10 katika mkoa wa Mtwara.
Mkuu wa kitengo cha kusaidia jamii cha Vodacom Tanzania(Vodacom Foundation) Reenu Verma amesema,“Vodacom Foundation kupitia mradi wake wa Girl Pawa imelenga kuwawezesha wasichana na wanawake kutimiza ndoto za maisha yao kwa kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowafanya wabaki nyuma baadhi yake zikiwa ni ukosefu wa elimu na kutojiamini na tumeamua kuongeza ufadhili ili mradi uweze kuwafikia wasichana wengi zaidi”
Kwa upande Meneja wa mradi huu wa T-MARC,Doris Chalambo alishukuru kwa ufadhili huu kwa kuwa utanufaisha wasichana wengi zaidi ya 5,784 walionufaika kwa awamu ya kwanza sasa idadi itaongezeka na kunufaisha wasichana wengine 4,200.
Katika awamu hii T-MARC itawapatia elimu ya kufundisha wasichana walimu wengine 20. Lengo la Mradi wa Hakuna Wasichoweza ni kuwapatia elimu ya uzazi,afya,kuwajengea uwezo wa kujiamini na kuwapatia Pedi za gharama nafuu watoto wa kike waliopo katika umri wa kuvunja ungo katika mkoa wa Mtwara ambapo idadi ya wasichana wanaohudhuria masomo mashuleni imeongezeka tofauti na siku za nyumba ambapo wasichana walipokuwa wanaingia katika hedhi wengi wao walikuwa wanashindwa kwenda mashuleni.
Mradi unatekeleza mpango wa taifa kwa vitendo wa kuhakikisha watoto wa kike hawabaki nyuma bali wanapata fursa sawa na wenzao wa kiume.
Elimu ya afya inawawezesha kujua athari za magonjwa mbalimbali na elimu ya uzazi inawawezesha kujua mabadiliko ya miili yao kutokana na makuzi ambapo wanaweza kuepuka kujiingiza kwenye vitendo vya ngono na kupata mimba za utotoni hali ambayo imekuwa ikisababisha idadi kubwa ya wasichana kushindwa kuendelea na masomo.
Awamu ya kwanza ya mradi huu ilifadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Watu wa Marekani (USAID) ambalo lilitoa ufadhili wa Dola za Kimarekani 200,000 na taasisi ya Vodacom Foundation ambayo ilitoa Dola za Kimarekani 100,000.
Chanzo: GLP
No comments:
Post a Comment