Breaking News

Monday, March 23, 2015

MREMBO AZIMISHWA USIKU

Dustan Shekidele, Morogoro
Duh! Wakati magari ya serikali yanatakiwa kupaki saa 12 jioni, wiki iliyopita mrembo mmoja mkazi wa jijini Dar ambaye jina lake halikupatikana mara moja amefanyiwa kitu mbaya ndani ya gari la serikali usiku mnene baada ya kuzimishwa kwa pombe kali kisha kunusurika kubakwa.
Mrembo huyo akiwa hoi.
Tukio hilo lililoshuhudiwa na Ijumaa Wikienda lilijiri mishale ya saa 6:00 usiku kwenye Baa ya Break Point iliyopo maeneo ya Msamvu kandokando ya Barabara ya Morogoro-lringa.
Habari zilizopatikana eneo la tukio zilieleza kwamba dereva wa gari hilo la serikali (namba za usajili zinahifadhiwa kwa sababu maalum) aliyefahamika kwa jina moja la Asenga ndiye aliyedaiwa kuhusika na tukio hilo kwa mrembo huyo aliyetoka naye Dar huku mwenyewe akiwa tilalila.
Baada ya kufotoa picha za tukio huku mrembo huyo akiburuzwa na jamaa hadi kwenye gari kabla ya kupoteza fahamu, mwanahabari wetu alifanya mahojiano na watu mbalimbali ili kupata tukio hilo kwa kina.
Kwa upande wake mhudumu wa baa hiyo aliyekuwa akiwahudumia wawili hao alisema:
”Awali waliagiza bia lakini baadaye mwanaume aliagiza pombe kali yenye thamani ya shilingi elfu 25 na kumlazimisha mrembo huyo kuinywa.
“Jamaa alipoona hivyo alianza kumburuza yule mrembo na kwenda kumlaza kwenye gari lakini watu wakiwemo walinzi walimuona hivyo akashindwa kufanya alichotaka kumfanyia,” alisema mhudumu huyo.

Gari la serikali lililohusika kwenye tukio hilo.
Akihojiwa na mwandishi wetu huku akirekodiwa, dereva huyo alikuwa na haya ya kusema:
”Mimi nimetoka wizarani Dar, nimekuja Moro kikazi.
“Huyu mrembo ni mchepuko wangu nimetoka naye Dar, nilipofika hapa ukumbini nikakutana na demu wangu wa siku nyingi.“Sasa ili niwe na yule wa siku nyingi nikaona nimleweshe huyu akizimika nile raha na yule mwingine.“Kwanza nimeona umepiga picha kesho nisafishie uniletee,” alisema Asenga akionekana ‘yupo nyingi kichwani’ bila kujua anazungumza na Kamanda wa Oparesheni Fichua Maovu wa (OFM) ya Global Publishers.
Baadaye jamaa huyo aliwaachia walinzi wamlinde mrembo huyo kisha akaendelea na starehe zake kabla ya kutimka na mwanamke huyo kwenye gari.Mathias Daud ambaye ni mlinzi wa baa hiyo alipotakiwa kuzunguzia tukio hilo alisema:“Huyu jamaa anachezea kazi, unajua angemfungia kwenye gari angemuua yule mwanamke.”
 Chanzo: GLP
Read more ...

Sunday, March 22, 2015

JOKATE AANGUSHIWA DUA NA WATOTO!

Imelda Mtema
Dua! Mwamitindo na mtangazaji ‘the big name’ Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’, ametembelea kituo cha watoto yatima kilichopo maeneo ya Ubungo jijini Dar kisha kuangushiwa dua ya nguvu na watoto wa madrasa.
Wikiendi iliyopita Jokate alifika kituoni hapo kutoa misaada mbalimbali huku akiwa amejitanda kichwa chake ambapo alijumuika na watoto hao naye akakaa kwenye mkeka ndipo akazungukwa na watoto hao yatima kisha kuombewa dua ili abarikiwe na mambo yake yaende vizuri.
“Nilifurahi kuombewa dua na watoto. Hata hivyo, mimi sioni kama kuna tatizo, kikubwa zaidi Mungu tunayemuabudu ni mmoja ambaye anamsikiliza kila mtu kwa hiyo hakuna shida mimi kuombewa Kiislam,” alisema Jokate ambaye wikiendi iliyopita ilikuwa ni ‘bethidei’ yake huku akizindua ngoma yake mpya ya Leo Leo.
Chanzo GLP
Read more ...

EL CLASICO: MATHIEU, SUAREZ WAPELEKA KILIO REAL MADRID

Cristiano Ronaldo akiifungia Real Madrid bao pekee katika dakika ya 31 ya mchezo.
Jeremy Mathieu akipiga mpira wa kichwa uliozaa bao la kwanza kwa Barcelona.
MABAO mawili yaliyofungwa na Jeremy Mathieu katika dakika ya 19 na Luis Suarez dakika ya 56 yameipa ushindi timu ya Barcelona dhidi ya mahasimu wao Real Madrid kwenye uwanja wao wa nyumbani Nou Camp usiku huu.
Katika mtanange huo wa La Liga, Barcelona wametoka kifua mbele kwa mabao 2-1 dhidi ya Real Madrid.
Bao la Real Madrid limewekwa kimiani na Cristiano Ronaldo dakika ya 31 ya mchezo.
Kwa matokeo hayo, Barcelona wamefikisha pointi 68 mbele ya Real Madrid wenye pointi 64.
Read more ...

MNYAMA AISAMBARATISHA RUVU SHOOTING TAIFA


Wachezaji wa Simba SC wakishangilia lao la kwanza lililofungwa na Ibrahim Ajibu kwa mkwaju wa penalti.
Mshambuliaji wa Simba SC, Emmanuel Okwi (25) akiipangua ngome ya Ruvu Shooting.
Kocha Mkuu wa Simba SC, Goran Kopunovic akishangilia ushindi na wachezaji wake.
WEKUNDU wa Msimbazi 'Mnyama' au Simba SC leo wameisambaratisha Ruvu Shooting baada ya kuibamiza kwa mabao 3-0 kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara iliyopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Simba SC wamewekwa kimiani na Ibrahim Ajibu, Awadhi Juma na Said Ndemla.
Chanzo: GLP
Read more ...

Friday, March 20, 2015

DIAMOND: HEE! MIMBA YA ZARI IMETOKA!

Na Musa Mateja
Mwanamuziki ambaye pia ni Rais wa Wasafi Classic Baby (WCB, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ameshangazwa na madai kuwa eti mimba ya mpenzi wake Zarina Hassan ‘Zari’ imetoka na kuwataka Wabongo kuacha tabia ya uzushi.

Nasibu Abdul ‘Diamond’ akiwa na mpenzi wake zari.

Akizungumzia madai yaliyokuwa yamezagaa mtandaoni kuwa ile mimba yake aliyokuwa akiilea kama yai kwa Zari imechoropoka, Diamond alisema:

“Hee! Eti mimba ya Zari imetoka! Wanaosema hivyo walaaniwe. Mbona Wabongo wazushi sana, itakuwaje hivyo halafu nisijue. Zari yuko fiti na mimba inaendelea vizuri, ona picha za kitumbo (anamuonesha paparazi picha za Zari kwenye simu yake).

“Kuna wapuuzi wachache tu wanakaa na kujitungia mambo yao ili wajenge mada zao, niliona sana watu wakijibizana na kubishana juu ya hilo, lakini nikutoe wasiwasi kuwa hakuna taarifa kama hizo.”
Chanzo: GLP
Read more ...

NAY AMFUMANIA MCHUMBA'KE KITANDANI

Musa mateja
KABAANG! Mkali wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, amedaiwa kumfumania ‘laivu’ mchumba wake Siwema akiwa kitandani na ‘serengeti boy’ wake ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja, Ijumaa lina full stori.
Mkali wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’.
NI MWANZA
Kwa mujibu wa chanzo kilichoshuhudia mwanzo mwisho, tukio hilo lilichukua nafasi Machi 15, mwaka huu maeneo ya Kitangiri jijini Mwanza ambako mrembo huyo alikuwa akiishi, baada ya Nay kupenyezewa ‘ubuyu’ kuwa mrembo huyo usiku wa Machi 14 alionekana akiponda raha ndani ya klabu moja iliyopo katika jengo la Hoteli ya Golden Crest.
“Wambeya walimpenyezea habari Nay, kesho yake asubuhi sana akatimba Mwanza kwa ndenge na kumkuta laivu Siwema akiwa na seregeti boy wake kitandani,” kilisema chanzo hicho kilichoomba hifadhi ya jina lake.
AMPOKONYA SIMU, AWAPIGA PICHA
Chanzo hicho kilizidi kumwaga data kuwa, Nay baada ya kuwakuta wawili hao wakiwa katika hali ya taharuki katika chumba cha nyumba hiyo ambayo alimpangishia Siwema, alimpokonya simu mpenzi wake huyo na kuwapiga picha za ushahidi wawili hao kisha akamchukua mwanaye kurudi Dar.
SIWEMA ATOKA NA KANGA MOJA
“Siwema baada ya kuona Nay amempokonya simu, alikurupuka akiwa na kanga moja kisha kumfuata ili arejeshewe simu yake, Nay aligoma na kukwea teksi akamuacha Siwema akilalama,” kilidai chanzo hicho.
NAY MSTARABU?
“Kiukweli Nay ni mstarabu sana maana hakuonyesha hasira za aina yoyote pamoja na kwamba aliwafuma laivu, alitoka taratibu, hakufanya ugomvi wowote kama watu wengine wanavyofanya pindi wanapofumania,” kilizidi kudai chanzo chetu.
NAY AKWEA PIPA, ARUDI DAR
Chanzo hicho kilizidi kudai kuwa, baada ya Nay kufanikiwa kumuacha Siwema na jamaa yake, alikwenda Uwanja wa Ndege wa Mwanza na kupanda ndege kurejea maskani kwake jijini Dar.
“Jamaa (Nay) hakutaka kuuweka usiku, alichokifanya ni kukwea pipa na kichanga chake hadi jijini Dar na kwenda kumkabidhi mama yake,” kilisema chanzo hicho.
Siwema.
NAY ANASEMAJE?
Mwanahabari wetu baada ya kuzinyaka habari hizo, alimvutia ‘waya’ Nay ambapo alipopatikana na kusomewa mashtaka ya kwenda kumfumania mchumba wake, alisema hayupo tayari kuzungumzia suala hilo kwa undani lakini akadai amemchukua mwanaye mikononi mwa Siwema kutokana na mchumba wake huyo kuzidiwa na mambo yake.
“Sitaki kuzungumzia chochote kwa sababu sitaki kuonekana mbaya, ila kiukweli nilienda Mwanza na kumchukua mwanangu na hapa ninapozungumza na wewe, mwanangu yupo chini ya uangalizi wa mama yangu mzazi,” alisema Nay.
SIWEMA KAFUATA SIMU YAKE
Wakati gazeti hili linakwenda mitamboni, chanzo kilicho karibu na wawili hao kilipenyeza ubuyu kuwa Siwema ameibuka jijini Dar kwa lengo la kufuata simu yake ikidaiwa kwamba eti ina siri zake nyingi.
SIWEMA HAPATIKANI
Jitihada za kumpata Siwema kupitia simu yake ili aweze kufunguka kwa upande wake hazikuzaa matunda kwani simu yake ilikuwa mikononi mwa Nay, jitihada zinaendelea ili na yeye afunguke ukweli wa tukio hilo.
TUJIKUMBUSHE
Nay na Siwema wamedumu kwenye uhusiano kwa takriban miaka mitatu ambapo wamefanikiwa kupata mtoto huyo mmoja. Awali, Nay aliwahi kuingia kwenye mgogoro na kigogo mmoja ambaye alikuwa akimtaka mrembo huyo lakini alifanikiwa kumuweka mikononi mwake kabla ya kumfumania na serengeti boy.
Chanzo: GLP
Read more ...

Monday, March 16, 2015

MOTO WAUNGUZA BWENI LA MABIBO HOSTEL JIJINI DAR

Wanafunzi wakijaribu kuokoa baadhi ya mali kutoka katika bweni la Block B kwenye hosteli ya Mabibo, Dar.
Moto ukiunguza bweni hilo.
Moshi mkali ukifuka kutoka katika bweni la Block B linaloendelea kuungua hivi sasa.
Wanafunzi wakishuhudia moto huo ukiendelea kuunguza bweni la Block B.
...wakitaharuki kutokea kwa moto huo.
....moto ukiendelea kuunguza bweni hilo.
Gari la zimamoto likiwasili eneo la tukio japo kwa kuchelewa.
Wanafunzi wakiwa nje ya jengo lililoungua wakati wakitafakari pakwenda.
Sehemu ya paa la jengo hilo iliyoungua.
Baadhi ya vitu vilivyookolewa.
Wafanyakazi wa Tanesco wakiwasiri eneo la tukio kutoa msaada.
Baadhi ya wanafunzi wakitafuta pakujihifadhi baada ya janga hilo.
Wanafunzi wakijadiliana jinsi ya kufanya.


MOTO mkali umeunguza bweni la Block B la hosteli ya Mabibo jijini Dar es Salaam muda huu. Chanzo cha moto huo na bado hakijafahamika.
Baadhi ya wanafunzi wanafanya jitihada za kuokoa mali zilizopo katika bweni hilo.

Moto mkubwa umezuka sehemu ya bweni la wanawake katika hosteli ya Chuo KiKuu cha Dar es Salaam lililopo Mabibo jijini Dar leo asubuhi na kusababisha vitu kadhaa kuungua pamoja na upotevu wa mali.
Katika tukio hilo wanafunzi wawili wamekimbizwa hospitali baada ya kuumia katika purukushani za kujiokoa ambapo mmoja alijirusha kutoka ghorofa ya pili ulipoanzia moto huo na mwingine aliumia kwenye mkanyagano wakati wa kujiokoa.
Chanzo: GLP


Read more ...

VODACOM FOUNDATION YAUPA JEKI $ 166,000 MRADI WA HAKUNA WASICHOWEZA

Wasichana kutoka kata ya Ufukoni mkoani Mtwara wakisubiri kupatiwa elimu ya Afya na uzazi na kugawiwa pedi kupitia mradi wa Hakuna Wasichoweza unaoendeshwa na taasisi ya T-Marc chini ya ufadhili wa USAID na Vodacom Foundation.Vodacom Foundation imeongeza $166,000 kwa ajili ya kuuongezea nguvu mradi huo unaowalenga wasichana wanafunzi waliopo mashuleni na wale wasio mashuleni na kwa kuanzia zoezi hili linafanyika katika mkoa Mtwara.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi ya Mwenge iliyopo mkoani Mtwara wakifurahi baada ya kugawiwa pedi za kujikinga wanapokuwa kwenye hedhi.Mpango huo wa kuwagawia wasichana pedi na kuwapatia elimu ya Afya na uzazi uko chini ya mradi wa Hakuna Wasichoweza unaoendeshwa na taasisi ya T-Marc chini ya ufadhili wa USAID na Vodacom Foundation.Vodacom Foundation imeongeza $166,000 kwa ajili ya kuuongezea nguvu mradi huo unaowalenga wasichana wanafunzi waliopo mashuleni na wale wasio mashuleni na kwa kuanzia zoezi hili linafanyika katika mkoa Mtwara.
Kutokana na mafanikio yaliyopatikana katika awamu ya kwanza ya mradi wa kuwawezesha wasichana wa Hakuna  Wasichoweza, taasisi ya Vodacom Foundation imeongeza ufadhili wa Dola za Kimarekani 166,000 ili mradi uendelee na uweze kuwafikia wasichana 4,200 katika shule nyingine 10 katika mkoa wa Mtwara.
Mkuu wa kitengo cha kusaidia jamii cha Vodacom Tanzania(Vodacom Foundation) Reenu Verma amesema,“Vodacom Foundation kupitia mradi wake wa Girl Pawa imelenga kuwawezesha wasichana na wanawake kutimiza ndoto za maisha yao kwa kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowafanya  wabaki nyuma baadhi yake zikiwa ni ukosefu wa elimu na kutojiamini na tumeamua kuongeza ufadhili ili mradi uweze kuwafikia wasichana wengi zaidi”
Kwa upande Meneja wa mradi huu wa T-MARC,Doris Chalambo alishukuru kwa ufadhili huu kwa kuwa utanufaisha wasichana wengi zaidi ya 5,784 walionufaika kwa awamu ya kwanza sasa idadi itaongezeka na kunufaisha wasichana wengine 4,200.
Katika awamu hii T-MARC itawapatia elimu ya kufundisha wasichana walimu wengine 20. Lengo la Mradi wa Hakuna Wasichoweza  ni kuwapatia elimu ya uzazi,afya,kuwajengea uwezo wa kujiamini na kuwapatia Pedi za gharama nafuu watoto wa kike waliopo katika umri wa kuvunja ungo katika mkoa wa Mtwara ambapo idadi ya wasichana wanaohudhuria masomo mashuleni imeongezeka tofauti na siku za nyumba ambapo wasichana walipokuwa wanaingia katika hedhi wengi wao walikuwa wanashindwa kwenda mashuleni.
Mradi unatekeleza mpango wa taifa kwa vitendo wa kuhakikisha watoto wa kike hawabaki nyuma bali wanapata fursa sawa na wenzao wa kiume.
Elimu ya  afya inawawezesha kujua athari za  magonjwa mbalimbali na elimu ya uzazi inawawezesha kujua mabadiliko ya miili yao kutokana na makuzi ambapo wanaweza kuepuka kujiingiza kwenye vitendo vya ngono na kupata mimba za utotoni hali ambayo imekuwa ikisababisha idadi kubwa ya wasichana kushindwa kuendelea na masomo.
Awamu ya kwanza ya mradi huu ilifadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Watu wa Marekani (USAID) ambalo lilitoa ufadhili wa Dola za Kimarekani 200,000 na taasisi ya Vodacom Foundation ambayo ilitoa Dola za Kimarekani 100,000.
Chanzo: GLP
Read more ...

MBUNGE FILIKUNJOME ATIMIZA PIA AHADI YA UJENZI WA DARAJA MTO KITEWAKA KWA TSH MILIONI 248, ASAIDIA VIFAA VYA UJENZI KWA TSH MILIONI 248

 Mbunge  Filikunjombe akilitazama daraja la mbao la mto Kitewaka ambalo litajengwa kisasa.
 Wannchi  wa  kijiji  cha Maholong'wa  wakimpongeza  mbunge  Filikunjombe kwa kutimiza ahadi yake.
 Waumini  wa  kanisa la Anglikana Maholong'wa Ludewa  wakimkabidhi zawadi mbali mbali mbunge Filikunjombe baada ya  kuwasaidia bati na  saruji  ya kutosha  kujenga kanisa  jipya.
 Viongozi wa kanisa la Anglikana na wa CCM Ludewa  wakiongozana na mbunge Filikunjombe  mwenye kofia.
 Mbunge  Filikunjombe akisaidi kupalilia mahindi katika shamba la mchungaji wa kanisa la Anglicana Maholong'wa baada ya  kufika  kusaidia ujenzi  wa kanisa  hilo.
 Mkutano wa mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe na  wanakijiji  wa Maholong'wa.
 Mzee  wa  kanisa la E.A.G.T Maboga  Ezekia Mhagama  (kulia)akimwombea  dua  mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe baada ya  kutoa misaada  mbali mbali ya ujenzi na  kujitolea kinanda  kwa  kanisa  hilo vyote  vikiwa na thamani ya zaidi ya Tsh milioni 11  wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Maholong'wa.
Mkurugenzi  Ludewa Bw Waziri akizungumza katika mkutano  wa Mbunge Filikunjombe.
 Wananchi  wa Maholong'wa wakimpokea mbunge  wao.
 Katibu mwenezi wa CCM mkoa wa Njombe Bw Honoratus Mgaya  akiwahutubia  wananchi wa Maholong'wa .
Na matukiodaimaBlog.
MBUNGE wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe ametimiza ahadi yake ya ujenzi wa daraja la mto  Kitewaka katika kijiji cha Maholong'wa kata hiyo ya Ludende baada  ya serikali kumpatia  kiasi cha Tsh milioni 2480 zilizokuwa zikihitajika kwa ajili ya ujezi wa daraja hilo .

Mbali ya  kutimiza ahadi hiyo ya  daraja  pia amechangia vifaa vya ujenzi vyeye thamani ya zaidi ya Tsh milioni 11 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa nyumba ya mwalimu katika shule ya Msingi Maholong'wa na ujenzi wa kanisa la Anglikana kijiji cha Maholong'wa kata ya Ludende wilayani Ludewa mkoani Njombe .

Akizungumza na wananchi hao leo mbunge Filikunjombe alisema kuwa kuwepo bungeni ni heshima ya wana Ludewa na kuwa hata vurugu kubwa ambazo amekuwa akizifanya bungeni si kwa maana nyingine zaidi ya kupigania maendeleo ya wananchi wake.

Hata   hivyo  aliipongeza  serikali  kuwa  kusaidia  kutoa  fedha   hizo  kwa  wakati kwa ajili ya  kuanza ujenzi hao na  kuwa  iwapo  asingefuatilia kwa karibu   serikalini ama angekuwa wa kulala bungeni yawezekana  fedha kwa  ajili ya ujenzi wa daraja   hilo zisingetolewa sasa.

 “wapo wabunge wengine ambao kazi yao ni kusinzia tu na wala haulizi swali …..ila huo pia ndio uwakilishi wake ulipoishia …..mimi silali kule bungeni mimi ninawatetea na kuwapiganieni kwa kulia nalia na kwenye kugombana nagombana pia pale kwenye kunyenyekea nanyenyekea….. napenda kuwaelezeni kuwa kazi ambayo mlinipa kuwawakilisha bungeni naitumia vema hadi sasa sijakwama kuwatumikia ….nilisema mwanzoni mimi navurugu bungeni ila ni vurugu za kimaendeleo”

Filikunjombe alisema kuwa waakati akiomba kuwa mbunge wa Ludewa alitaka kuwawakilisha bungeni na kushirikiana nao katika shughuli za kimaendeleo hivyo angekuwa mbunge wa ajabu kama angekuwa mbali na shughuli za kimaendeleo katika jimbo lake .

 Alisema wakati akigombea ubunge mwaka 2010 aliwaahidi wananchi wa kata la Ludende kuwajengea daraja la kisasa zaidi katika kijiji cha Maholong'wa ili kuchochea kasi ya maendeleo katika kata ya Ludende na kata za jirani ,ahadi ambayo sasa anaitimiza kwa kumpata mkandarasi atakayejenga daraja hilo kwa Tsh milioni 248 na ujenzi wake utaanza mara moja baada ya mvua kutulia . “

"Mimi nataka ujenzi huu uanze mara moja kwani kama shida wananchi wangu mmetesema sana hivyo sasa nataka iwe basi matesa na sitapenda kuona Halmashauri inaziweka pesa hizo pasipo kutumika kwa kazi iliyokusudiwa fedha  za ujenzi huu zimetoka serikalini baada ya kuwabana zaidi"

Alivitja vifaa hivyo kuwa ni bati 200 na saruji 200 pia kinanda kwa kanisa la E.A.G.T na vifaa mbali mbali vya michezo pamoja na kuwakodia usafiri kutoka Dar es Salaam hadi kijijini hapo kwa ajili ya kusafirisha vifaa hivyo.

 Awali viongozi wa madhehebu ya dini na vyama vya siasa katika kata ya Ludende wilaya ya Ludewa wamepongeza jitihada kubwa zinazofanywa na mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe na kuwa hawahitaji kubadili tena wabunge kama nguo .

 Huku mwenyewe akidai kuwa yeye si mbunge wa kusinzia bungeni ni makini katika kuwawakilishi wananchi wake na kuwa ana vurugu sana bungeni ila vurugu zake ni za kimaendeleo si vinginevyo.

Wakishukuru mara baada ya kuwakabidhi mkandarasi wa kuanza ujenzi wa daraja , pamoja na saruji na bati kwa ajili ya kuchangia miradi mbali mbali ya kimaendeleo katika kata hiyo na ujenzi wa kanisa jipya ya Anglicana kijiji cha Maholong’wa.

 Viongozi hao akiwemo mzee wa kanisa la E.A.G.T Mboga Bw Ezekia Mhagama na mkuu wa shule ya msingi Maholong’wa Bw Damas Malihayi walisema kuwa maendeleo makubwa yanayoendelea kuonekana katika wilaya ya Ludewa ni jitihada kubwa ambazo zinafanywa na mbunge huyo na hivyo wao kama viongozi wa dini kazi kubwa ni kuzidi kumwombea afya njema ili aendelee kuwa mbunge wa jimbo hilo kwa vipindi vingine zaidi.

 Alisema mzee huyo wa kanisa la E.A.G.T kuwa matumaini ya wananchi wa Ludewa yamekuwa makubwa zaidi dhidi ya mbunge wao kutokana na sura ya Ludewa kwa sasa baada ya mateso ya miaka zaidi ya 50 ya Uhuru bila kuwepo kwa maendeleo yanayoonekana ila toka alipoingia mbunge Filikunjombe mwaka 2010 wananchi wa Ludewa ndipo walipata uhuru wao na kuwa wao wanajiona kama miaka hii mitano toka walipomchagua mbunge huyo kuwa mbunge wao ndipo wao walipopata uhuru wao.

“Tunatambua nchi yetu ilipata uhuru mwaka 1961 kwa maeneo mbali mbali ya nchi wananchi wake kusogezewa huduma mbali mbali zikiwemo barabara za lami ila sisi Ludewa lami tumeanza kuiona mwaka jana na kama huku Maholong’wa daraja ambalo ni tegemeo kubwa kwetu lilikuwa la mbao hadi sasa ambapo mbunge wetu ametusaidia kutafuta pesa ya kujenga daraja la kisasa na huu ndio uhuru wetu “

Mhagama alipongeza pia kwa msaada wa saruji na bati za kutosha kukamilkisha ujenzi wa kanisa la Anglicana na msaada wa kinanda kwa kanisa lake la E.A.G.T kuwa ni mbunge pekee kusaidia jamii nzima ya Ludewa pasipo kutazama masuala ya itikadi zao .

 Hivyo allisema kwa wananchi wa Ludewa hawana sababu ya kuendelea kubadili badili wabunge kwa sasa kwani utendaji kazi wa mbunge Filikunjombe umewakuna wengi na hivyo kazi kubwa kwao ni kuendelea kumuunga mkono kwa kumpitisha tena na tena kuwa mbunge wao .

 Mkuu wa shule ya Msingi Maholong’wa Bw Malihayi alisema kuwa kuna haja ya wana Ludewa kushikamana na kuona hawampotezi mbunge huyo na badala yake kuzidi kumpa ushirikiano zaidi.

Kwa upande wake Paschal Kayombo akizungumza kwa niaba ya vijana wa kata hiyo alisema kuwa kero kubwa ya vijana ilikuwa ni daraja hilo la mto Maholong’wa ambalo kwa sasa limekwisha patiwa ufumbuzi na kuwa vijana kwa sasa wanaimani kubwa na utendaji kazi wa mbunge huyo.

Katibu mwenezi wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Njombe Honoratus Mgaya akiwahutubia wananchi hao alisema kuwa CCM ni chama kizuri sana ila wanaofanya wananchi kukichukia chama ni baadhi ya viongozi wakiwemo wabunge ambao wameshindwa kuwatumikia vema wananchi wao.

Kwani alisema iwapo kila mbunge atafanya kazi kwa kujituma kama ilivyo kwa mbunge Filikunjombe uwezekano wa kata ama majimbo kuchukuliwa na vyama vya upinzani usingekuwepo ila wanaopigia kura wapinzani ni wana CCM ambao wamechoshwa na uwajibikaji mbovu wa wale waliowachagua.
Chanzo: GLP
Read more ...

IDD AZZAN ATOA MSAADA WA KITI CHA MAGURUDUMU KWA MLEMAVU JIMBONI KWAKE‏

Pichani ni Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Mh. Iddi Azzan akikabidhi kiti maalum cha kujisaidia pamoja na kiti cha magurudumu kwa mama huyo mlemavu.
Na Modewji Blog Team
Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Mh. Iddi Azzan (CCM) ametoa msaada wa kiti cha magurudumu kwa Rehema Nditi mkazi wa Magomeni Mwembe Chai kama msaada kutokana na taabu aliyokuwa akiipata.
Idd Azzan ametoa msaada … ambapo baada ya kuona Rehema Nditi kupataa tabu ya kukosa kiti hicho.
Mbunge huyo amekua akisaidia maendeleo mbalimbali ikiwemo shughuli za kijamii ndani ya jimbo lake hilo.
Aidha, Mh. Iddi Azzan ametoa rai kwa Watanzania kuungana nae katika kuchangia pesa kwa ajili ya kununua Bajaji ambayo itafanya biashara ili waweze kuendesha maisha ya kila siku.
“Watanzania tuungane kumchangia mama huyu kiasi chochote ilikununua bajaji kwa ajili ya kufanya biashara ili waweze kuendesha maisha yao ya kila siku kupitia kipato cha biashara hiyo ya Bajaji” alieleza Idd Azzan.
Kwa upande wake, Mtangazaji wa kipindi cha "Mimi na Tanzania, Kinachoerushwa na kituo cha Channel Ten, Hoyce Temu amefungua michango hiyo kwa kutoa kiasi cha Tsh. 500,000/- ili kuhamasisha na wengine kuchangia.
Michango hiyo inaweza kuwasilishwa kwenye ofisi za Mbunge wa jimbo la Kinondoni ama unaweza kuwasiliana moja kwa moja na Rehema Nditi
Chanzp : GLP
Read more ...

Friday, March 13, 2015

MAKALIO YAMPAISHA MASOGANGE MAREKANI

Na Hamida Hassan/Ijumaa
Staa  aliyejipatia umaarufu mkubwa kutokana na makalio yake, Agnes Gerald ‘Masogange’ sasa amepaa kimataifa zaidi na kuwa  gumzo hadi Marekani baada ya hivi karibuni mtandao mmoja wa watu maarufu nchini humo kumpa shavu.
Staa  aliyejipatia umaarufu mkubwa kutokana na makalio yake, Agnes Gerald ‘Masogange’.
Masogange aliripotiwa na mtandao wa Media Take Out na kumuelezea kuwa ni staa mwenye makalio makubwa barani Afrika akitokea Tanzania.Mbali na maelezo kibao ya kusifia wowowo lake, mtandao huo uliposti picha kibao za mwanadada huyo ambaye sasa anaishi Afrika Kusini akiweka mapozi tofauti ya kimitego.
Hata hivyo, baadhi waliponda maelezo hayo kwa kusema kuwa, Afrika ina mabinti wenye maumbo tata kuliko Masogange hivyo mtandao huo ungefanya uchunguzi kabla ya kuripoti habari hiyo.
Chanzo: GLP
Read more ...

New Video" Linex Ft Diamond - Salima

11005034_1561403867474813_1096267481_n 
Video mpya kutoka kwa Linex akimshirikisha Diamond "Salima"



Read more ...

New Video - Ommy Dimpoz - Wanjera

 Ommy na wema
 Ile video iliyokuwa inasubiliwa kwa hamu na wapenzi wa msanii wa Bongo Flaver Ommy Dimpoz " Wanjera" Kwenye video hiyo Wema Sepetu amecheza kama mpenzi wa Ommy Dimpoz

Read more ...

Wednesday, March 11, 2015

WEMA, HEMED KUTOA ‘MAPENZI YAMEROGWA’ KARIBUNI

Waigizaji Wema, Hemed, Neema na wengine wakiwa katika harakati za kurekodi filamu hiyo.
MWIGIZAJI Wema Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ na mtanashati wa Bongo Movies, Hemed Suleiman ‘PhD’ wamekutana katika kushuti muvi moja inayokwenda kwa jina la ‘MAPENZI YAMEROGWA’, kazi ambayo inaendelea kwa umakini katika maeneo ya Kinondoni…
Waigizaji Wema, Hemed, Neema na wengine wakiwa katika harakati za kurekodi filamu hiyo.
MWIGIZAJI Wema Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ na mtanashati wa Bongo Movies, Hemed Suleiman ‘PhD’ wamekutana katika kushuti muvi moja inayokwenda kwa jina la ‘MAPENZI YAMEROGWA’, kazi ambayo inaendelea kwa umakini katika maeneo ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Wema, filamu hiyo ambayo pamoja na waigizaji wengine, imemshirikisha pia mwigizaji maarufu, Neema,  itaonyesha ni jinsi gani mapenzi yanavyowachanganya wahusika.
Chanzo: GLP
Read more ...
Designed By VungTauZ.Com