Breaking News

Saturday, July 16, 2016

MOJA KWA MOJA: Yanayojiri kuhusu 'mapinduzi' Uturuki

Mapinduzi07:15 Shirika la Reuters limemnukuu afisa wa serikali ya Uturuki akisema watu zaidi ya 60 wamefariki naye waziri wa haki anasema 336 wanazuiliwa kufuatia jaribio la mapinduzi ya serikali.
07:13 Afisa katika afisi ya rais wa Uturuki amesema ndege za kivita aina ya F-16 zinatumiwa kuwashambulia wanajeshi wa mapinduzi wenye vifaru ambao wamekuwa nje ya ikulu ya rais mjini Ankara.
07:10 Wanajeshi karibu 50 ambao walihusika katika jaribio la mapinduzi, wamejisalimisha katika daraja la Bospherus, shirika la habari la Reuters limeripoti, na kuongeza kwamba wanajeshi wengine walijisalimisha katika uwanja wa Taksim Square mjini Istanbul.

Erdogan arejea Istanbul

04:30 Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amejitokeza katika uwanja wa ndege wa Istanbul, akiwa amezingirwa na mamia ya wafuasi baada ya kundi la wanajeshi kujaribu kupindua serikali yake.
Kwenye kikao cha dharura na wanahabari, ameahidi kusafisha jeshi na akaahidi kwamba wote waliohusika wataadhibiwa vikali.
Kundi la wanajeshi lilikuwa limetekeleza jaribio la kupindua serikali.
Taarifa kutoka kwa kundi hilo la jeshi, ambayo ilisomwa kupitia runinga ya taifa ilisema jeshi lilikuwa limechukua mamlaka.


Image copyrightREUTERS
04:06 Jaribio la mapinduzi 'limefeli'
Msemaji wa idara ya ujasusi ya Uturuki, MIT, amesema jaribio la kupindua serikali limefeli lakini bado kuna wanajeshi kadha wanaoendelea kupigana.
"Watu wanayaandama makundi haya. Wote walioshiriki watashtakiwa uhaini. Kwa sasa, hakuna tatizo lolote," Bw Nuh Yilmaz amenukuliwa na tovuti ya habari ya Hurriyet.
04:01 RaisRecep Tayyip Erdogan amerejea Istanbul na kwa mujibu wa vyombo vya habari, ameonekana miongoni mwa wafuasi wake nje ya uwanja huo. Amesema waliohusika watakabiliwa vikali, bila kujali wanafanyia kazi taasisi gani.
04:00 Shirika la habari la Reuters linasema karibu wanajeshi 30 wa Uturuki wamesalimisha silaha zao baada ya kuzingirwa na maafisa wa polisi katika uwanja wa Taksim Square, Istanbul.
03:58 Kundi la wanajeshi laingia afisi za kituo cha televisheni chaCNN-Turk TV, ambacho ni kituo cha kibinafsi, na kuzima matangazo ya kituo hicho.
03:57 Mkuu wa polisi wa Istanbul amenukuliwa akisema wanajeshi walioshiriki jaribio la mapinduzi walikuwa 104. Anasema kiongozi wao amekuwa Kanali Muharrem Kose.
03:56 Ndege iliyombeba Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan imetua Istanbul, maafisa wameambia mashirika ya habari ya Reuters na AFP.
03:27 Waziri Mkuu wa Uturuki Binali muda mfupi uliopita amesema hali Uturuki kwa kiwango kikubwa imedhibtiiwa, na kuongeza kwamba jaribio la mapinduzi lilitekelezwa na wafuasi wa Fethullah Gulen.
Ameambia runinga ya NTV kwamba marufuku ya ndege kutopitia anga ya Ankara imetangazwa.


Image copyrightREUTERS

03:25 Kundi tiifu kwa mhubiri wa Kiislamu aishiye Marekani Fethullah Gulen limeshutumu jaribio la mapinduzi ya serikali nchini Uturuki na pia likashutumu madai ya wafuasi wa rais kwamba kundi hilo lilihusika.
03:03 Shirika la habari la Reuters linaripoti kuwa runinga ya taifa ya Uturuki, TRT imerejea hewani.
Taarifa zinadokeza kwamba huenda Rais Erdogan anasubiriwa uwanja wa ndege wa Ankara.
03:00 Shirika la habari laAnadolu linaripoti kuwa wafuasi wa serikali ya Uturuki, wakiongozwa na waziri wa wafanyakazi Suleyman Soylu, wameingia afisi za runinga ya taifa TRT.
Anadolu pia wanaripoti kuwa bomu limelipuliwa katika majengo ya bunge Ankara



02:49 Rais wa Marekani Barack Obama amehimiza pande zote Uturuki kuunga mkono "serikali iliyochaguliwa kidemokrasia Uturuki, kuonyesha uvumilivu, na kujizuia na vurugu au umwagikaji wa damu," ikulu ya White House imesema.
02:48 Kamanda wa kikosi cha wanajeshi maalum Jenerali Zekai Aksakalli, ameambia kituo cha televisheni cha NTV kwa njia ya simu kwa "wanaojaribu kupindua serikali hawatafanikiwa". "Watu wetu wanafaa wafahamu kwamba tutadhibiti hili ... Tumedhibiti hali."
02:46 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amehimiza kuwepo kwa utulivu Uturuki.
"Katibu mkuu anafuatilia kwa karibu matukio Uturuki. Anafahamu kuhusu taarifa za kutokea jaribio la kupindua serikali nchini humo," msemaji wake Farhan Haq amesema.
02:15 Shirika la habari la serikali la Anadolu linaripoti kuwa maafisa 17 wa polisi wameuawa kwenye shambulio la kutoka angani kituo cha polisi maalum cha Golbasi mjini Ankara.
02:14 Shirika la utangazaji la NTVla Uturuki limeripoti kwamba helikopta aina ya Sikorsky iliyokuwa inatumiwa na kundi lililojaribu kupindua serikali imedunguliwa na ndege ya kivita ya jeshi la Uturuki aina ya F-16.


Image copyrightGETTY

01:56 Waziri mpya wa mambo ya nje wa Uingereza Boris Johnson amesema amesikitishwa sana na yanayojiri Uturuki. Amesema ubalozi wa Uingereza nchini Uturuki unafuatilia yanayojiri na kuwataka raia wa Uingereza nchini humo kufuata ushauri utakaotolewa.


Image copyrightTWITTER

01:55 Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry amesema anatumai kutakuwa na amani, uthabiti na uendelevu nchini Uturuki, shirika la habari la Reuters limeripoti.
01:53 Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov amesema ni muhimu sana "kuzuia umwagikanji" wa damu Uturuki. Mambo yanafaa kutatuliwa kupitia mfumo wa kikatiba, amesema.
01:51 Ubalozi wa Marekani nchini Uturuki umewatahadharisha raia wake wawe. Wameshauriwa wakae maeneo salama, wajulishe jamaa na marafiki kwamba wako salama, lakini wasiende ubalozini au afisi za ubalozi kwa sasa.
01:50 Wanajeshi walio kwenye vifaru wanaonekana katika baadhi ya barabara za mji wa Ankara.


Image copyrightGETTY

01:47 Naibu waziri mkuuNuman Kurtulmus amesema moja kwa moja kupitia runinga kwamba chama tawala cha AK bado kinadhibiti nchi.
01:41 Shirika la habari la kibinafsi la Dogan linaripoti kwamba vjeshi limetuma vifaru nje ya majengo ya bunge, Ankara kwa mujibu wa shirika la habari la AFP.
01:39 Mwanahabari wa NTV ya Uturuki Oz Katerji ambaye amekuwa Taksim Square, Istanbul anasema jeshi limejaribu kuchukua udhibiti wa eneo hilo.
01:38 Wafuasi wa RaisErdogan walijitokeza Taksim Square katikati mwa Istanbul baada ya ripoti za jaribio la mapinduzi ya serikali kutokea.
Baadaye kumeripotiwa makabiliano katika uwanja huo, baadhi ya watu kwenye Twitter wakisema ufyatulianaji wa risasi umesikika karibu na uwanja huo.
01:37 Mbunge mmoja wa upande wa serikali ametumia BBC picha akisema watu wameanza kukusanyika karibu na majengo ya bunge mjini Ankara.

01:10 Kuna 'Mfumo sambamba' Uturuki? Rais Recep Tayyip Erdogan kwenye mahojiano yake na idhaa ya Uturuki ya CNN ameshutumu alichotaja kuwa "mfumo sambamba" kwa yaliyotokea leo.Inaaminika alikuwa akirejelea wafuasi wa Fethullah Gulen, mhubiri wa Kiislamu mwenye makao yake Marekani, ambaye Bw Erdogan amekuwa akimtuhumu awali kwa kuhusika katika majaribio ya mapinduzi ya serikali.



01:19 Erdogan 'alikuwa likizoni Marmaris'Rais Recep Tayyip Erdogan inadaiwa alikuwa likizoni katika mji wa Marmaris kwenye bahari ya Mediterranean jaribio la mapinduzi lilipotekelezwa.


ErdoganImage copyrightGETTY
Image captionBw Erdogan alizungumza na kituo cha CNN Turk kupitia Facetime

01:06 Shirika la habari la Anadolu limeandika kwenye Twitter kwamba milio ya risasi imesikika karibu na ikulu ya rais. Linasema watu walioshuhudia wanasema helikopta za kijeshi ndizo zilizofyatua risasi.



00:57 Twitter, Facebook, YouTube zazimwa



Image copyrightGETTY

00:55 Mlipuko mkubwa Ankara

Shirika la habari la AFP linasema mlipuko mkubwa umesikika Ankara. Duru za Kimarekani zimefahamisha Reuters kwamba milio ya risasi imesikika karibu na makao makuu ya mkuu wa jeshi la Uturuki mjini Ankara.



00:54 Runinga ya taifa ya Uturuki TRT haimo hewani tena, shirika la Reuters limeripoti. Awali, wanajeshi walidaiwa kuchukua udhibiti wa kituo hicho na mtangazaji akatangaza kuanza kutekelezwa kwa sheria za kijeshi.
00:50 Waziri Mkuu wa Uturuki Binali Yildirim ameandika kwenye Twitter kwamba nchi hiyo "haitavumilia daima vitendo vya ukiukaji wa sheria" na haitaruhusu demokrasia kuvurugwa.
00:47 Erdogan ataka Waturuki wajitokeze barabarani
Rais Recep Tayyip Erdogan ameambia kituo cha habari cha CNN Turk, kwenye mahojiano ya webcam, kwamba kitendo cha leo kimechochewa na kuwepo kwa "mfumo sambamba". Amesema jaribio la mapinduzi litakabiliwa kwa "hatua ifaayo" na kuwataka raia wa Uturuki wajitokeze barabarani.



00:45 Jeshi la Uturuki limetangaza kuanza kutekelezwa kwa sheria za kijeshi na kutangaza amri ya kutotoka nje, mtangazaji katika runinga ya taifa TRT ametangaza.
00:44 Vifaru zinadaiwa kuziba viwanja vya ndege vya Istanbul na Ankara. Safari zote za ndege za kimataifa uwanja mkuu wa ndege wa Istanbul zimesitishwa.
00:42 Wanajeshi wameingia katika afisi za runinga ya taifa ya Uturuki, TRT, mmoja wa wanahabari wa shirika hilo ameambia Reuters.
00:40 Duru katika afisi ya Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan zimeambia shirika la habari la Reuters na kituo cha runinga cha CNN Turk kwamba yuko salama. Hata hivyo, haijulikani alipo.


Image copyright.

00:31 Kundi moja la jeshi nchini Uturuki limetoa taarifa na kusema kwamba limepindua serikali ya nchi hiyo. Waziri mkuu Binali Yildirim akihutubu kwenye runinga amesema hatua ya kijeshi iliyochukuliwa na kundi moja haifai kuchukuliwa kama mapinduzi.


Image copyright

No comments:

Designed By VungTauZ.Com