
Usiku wa July 17 2016 kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom ambayo ndio wadhamini wakuu wa Ligi Kuu soka Tanzania bara, walitangaza na kutoa tuzo 13 kwa wachezaji, refa na timu bora zilizofanya vizuri msimu wa 2015/2016, Vodacom kwa kushirikiana na TFF wamefanikiwa kuchagua na kutoa zawadi kwa washindi wa tuzo hizo.

Washindi wa tuzo Ligi Kuu katika picha ya pamoja na wageni waalikwa
List ya washindi wa tuzo na zawadi walizochukua
- Mchezaji bora wa Ligi Kuu 2015/2016 ni Juma Abdul wa Yanga Tsh Milioni 9,228,820
- Mchezaji bora wa kigeni ni Thabani Kamusoko wa Yanga Tsh Milioni 5,742,940
- Mfungaji bora ni Amissi Tambwe wa Yanga Tsh Milioni 5,742,940
- Mchezaji bora chipukizi ni Mohamed Hussein wa Simba Tsh Milioni 4.
- Golikipa bora ni Aishi Manula wa Azam FC Tsh Milioni 5,742,940
- Refa bora ni Ngole Mwangole Tsh Milioni 5,742,940
- Kocha bora ni Hans van Pluijm wa Yanga Tsh Milioni 8.
- Timu yenye nidhamu Mtibwa Sugar Tsh Milioni 17,228,820
- Bingwa wa Ligi Kuu Yanga Tsh Milioni 81,345,723
- Mshindi wa pili Azam FC Tsh Milioni 40,672,861
- Mshindi wa tatu Simba Tsh Milioni 29,052,044
- Mshindi wa nne Tanzania Prisons Tsh Milioni 23, 241,635
- Mfungaji wa goli bora ni Ibrahim Ajib wa Simba Tsh Milioni 3

Kocha wa Yanga Hans van Pluijm baada ya kutwaa tuzo ya kocha bora akisalimiana na waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba

Kocha wa Yanga Hans van Pluijm akipokea tuzo ya kocha bora akiwa kaongozana na mkewe.

Kocha wa Yanga Hans van Pluijm akisalimiana na Rais wa TFF Jamal Malinzi

Mwameja akikabidhi tuzo ya golikipa bora kwa Aishi Manula wa Azam FC

Ibrahim Ajib akipokea mfano wa hundi ya Tsh Milioni 3 kama zawadi ya ufungaji goli bora.

Thabani Kamusoko akiwa na mkewe na mtoto wake alipopokea mfano wa hundi ya Tsh Milioni 5 kama zawadi ya mchezaji bora wa kigeni.

Kutoka kushoto ni Mohamed Hussein wa Simba ambaye ameshinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi.

Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba akimkabidhi tuzo ya mchezaji bora wa Ligi Kuu Juma Abdul wa Yanga

Kutoka kushoto ni mkuu wa masoko wa Yanga Omar, Juma Abdul na golikipa wa Yanga Deogratus Munish









Kamusoko na familia yake

Chanzo: millardayo.com
No comments:
Post a Comment