Breaking News

Saturday, July 16, 2016

PICHA 5: Gari jipya ya Cristiano Ronaldo aliyoinunua Tsh bilioni 4.9


Baada ya michuano ya Euro 2016 kumalizika na timu ya taifa ya Ureno inayoongozwa na nahodha wake Cristiano Ronaldo kutwaa taji hilo, headlines zimekuwa nyingi baada ya staa huyo kushinda Kombe hilo kwa mara ya kwanza katika historia ya maisha yake.
364CEF2B00000578-0-image-a-5_1468572305384
Ronaldo baada ya kutwaa Euro 2016 aliripotiwa kutoa msaada bonansi yake yote aliyopewa, ila headlines za staa huyo hazijaishia hapo, kwani ameamua kununua gari jipya ikiwa siku chache zimepita toka afanikiwe kutwaa Kombe la Euro 2016, kitendo ambacho kinatafsirika kama kuamua kujizawadia zawadi hiyo.
364CEF3300000578-0-image-m-4_1468572294471
Staa huyo wa Real Madrid amenunua gari aina ya Bugatti Veyron 16.4 Grand Sport, gari ambalo lina thamani ya pound milioni 1.7 kiasi ambacho ni zaidi ya bilioni 4.9 za kitanzania, gari aina ya Bugatti Veyron 16.4 Grand Sport aliyoinunua Ronaldo zinatajwa kuwa hadi sasa zimetengenezwa 450 tu, hiyo inatokana na thamani ya gari yenyewe.
364E03A700000578-3691646-image-m-16_1468577798661

No comments:

Designed By VungTauZ.Com