Breaking News

Saturday, July 16, 2016

PICHA: Kama ulisikia mradi wa zaidi ya Bilioni 85 wa Ronaldo, umefikia hapa

Staa wa timu ya taifa ya Ureno na klabu ya Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldoambaye pia ni mshindi wa tuzo tatu za Ballon d’Or, ameripotiwa kuandaa dola milioni 40 kwa ajili ya kufanya uwekezaji mkubwa wa biashara binafsi nje ya soka.
Ronaldo anaripotiwa kutumia zaidi ya dola milioni 40 ambazo ni zaidi ya bilioni 80 za kitanzania kwa ajili ya kuanzisha mradi wa hoteli, ambazo zitajengwa katika miji ya New YorkLisbonMadeira Funchal na Madrid kwa kushirikiana ubia na Pestana Hotels, mpango huo wa Ronaldo umeandikwa na Forbes.
rona 2
Ronaldo na Dionísio Pestana ambaye ni mshirika mwenzake katika biashara hiyo, wote wamezaliwa na kukulia Maideira Ureno, hivyo hiyo ni project ambayo inahusisha watu marafiki wawili na hotel yao ya kwanza itazinduliwa weekend hii Madeira, hoteli hizo bado zitaendelea kutumia jina la kibiashara la Ronaldo CR7.
“Kazi yangu ni kucheza soka lakini maisha siku zote hayawezi kuendelea kuwa kama hivi, nimeamua kuingia katika mradi huu kutokana nina timu kubwa ya watu wanaonizunguuka duniani, mimi bado kijana na nimetimiza au nimefanikiwa katika kila kitu, hivyo naandaa maisha yangu, mwanangu na familia yangu kwa miaka ya baadae” >>>Ronaldo

No comments:

Designed By VungTauZ.Com